Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Samson Guyo,
Hisia mseto zinazidi kuibuliwa kuhusiana na kauli ya Waziri wa Elimu Prof George Magoha kuwa ni lazima wazazi walipe karo ya shule ya muhula wa 3 la sivyo watoto warejeshwe manyumbani.
Baadhi ya wazazi waliozungumza na idhaa hii mjini Marsabit wametaja kuwa serekali haifai kulazimisha wazazi kulipa karo kwani idadi kubwa ya wazazi waliadhirika na janga la korona lilioadhiri kazi na hata biashara zao.
Baadhi yao wametaja kuwa Wizara ya elimu haifaia kuwaorodhesha wazazi kwa misingi ya kipato chao.
Vilevile wamekashifu vikali kauli ya Waziri huyo wa elimu kuwa wazazi wengine kutoka kwa familia zinazojiweza wamesusia kulipa karo kwa kisingizio cha kuadhiriwa na janga la korona wakiitaja kauli kama isiyo na misingi yeyote.
Akihutubu hiyo jana katika chuo kikuu cha JKUAT waziri Magoha aliwataka walimu wakuu kukagua kwa kina orodha ya wanafunzi na kubaini wanafunzi wanaotoka katika familia maskini na wale walio na uezo wa kulipa karo na kuwachukulia hatua zinazofaa.