Understanding Elavil: Uses, Benefits, and Safety
December 26, 2024
By Samuel Kosgei,
Gavana wa Marsabit Mohammud Ali amekashifu vikali Idara ya usalama katika kaunti ya Marsabit kwa madai ya kuzembea kazini na kuchangia kudumu kwa machafuko na mauaji ya kila mara katika jimbo la Marsabit.
Akizungumza katika hafla ya kuzindua kliniki ya saratani katika hospitali kuu ya Marsabit, Ali amedai kuwa kwa muda sasa pamekuwa visa vya uhalifu vya kujirudia ilhali idara ya usalama imelala kazini huku watu wakiuawa bila hatua mwafaka kuchuliwa.
Gavana Mohamud aidha amedai kuwa polisi imekuwa ikipendelea upande mmoja katika vita dhidi ya uhalifu katika jimbo hili. Ametolea mfano kisa cha majuma kadhaa ambapo watu wanne walikamatwa na bunduki kwenye gari la kaunti katika eneo la Elle Borr kaunti ndogo ya Turbi akisema polisi wamekuwa wakichukua hatua kwa mapendeleo.