County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Baadhi Ya Walimu Wa Shule Za Umma Kaunti Ya Marsabit Waelezea Kusikitishwa Kwao Na Hali Ya Shule.

Piicha;Hisani

By Adano Sharawe, Samwel Kosgei & Adho Isacko

Baadhi Ya Walimu Wa Shule Za Umma Kaunti Ya Marsabit Wameeleza Kusikitishwa Kwao Na Hali Ya Shule Wanaozoongoza Ikizingatiwa Kuwa Wanahitajika Kuzingatia Masharati Ya Wizaraya Afya Ilhali Hawajapokezwa Pesa Za Shughuli Hiyo Na Serikali Kama Walivyoahidiwa.

Baadhi Ya Changamoto Wanazotaja Kuzipitia Ni Uchache Wa Madarasa Huku Wanafunzi Wakiongezeka, Uchache Wa Madawati Hivyo Kufanya Sharti Ya Kukaa Umbali Wa Mita Moja Unusu Kwa Wanafunzi Shuleni Kuwa Vigumu.

Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya Karare Mixed Joseph Malmalo Amesema Kuwa Wao Kama Shule Bado Wanasubiria Maelekezo Kutoka Kwa Wakuu Wa Wizara Ya Elimu Jimboni Ili Kufahamu Hatma Ya Kusuluhisha Uchache Wa Madarasa.

Uongozi Wa Shule Ya Upili Ya Moi Girls Jimboni Marsabit Nayo Imesema Kuwa Kutokana Na Idadi Kubwa Ya Wanafunzi Shuleni Humo Itabidi Watumie Darasa Moja La Ukumbi Wa Wanafunzi Kama Sehemu Ya Kulalia Kwani Itakuwa Vigumu Mabweni Yao Kuwa Na Umbali Unaohitajika. Shule Hiyo Ina Jumla Ya Wanafunzi 700. Jerry Onyango Ni Mwalimu Kutoka Shule Ya Upili Ya Moi Girls.

Katika Shule Ya Msingi Ya North Horr Mjini Noth Horr Naibu Mwalimu Mkuu Wa Shule Hiyo Konchora Boru Ameshikilia Kuwa Shule Hiyo Inayo Idadi Kubwa Zaidi Ya Wanafunzi Na Kwamba Umbali Wa Mita Moja Miongoni Mwa Wanafunzi Itasalia Kuwa Tatizo.

Kulingana Na Mwalimu Boru Shule Hiyo Inayo Jumla Ya Wanafunzi 634 Shuleni Humo Ambapo 471 Tayari Wameripoti Na Kwamba Kudumisha Umbali Wa Mita Moja Itakuwa Ndoto.

Mw. Boru Anahoji Kuwa Ikiwa Umbali Wa Mita Moja Utazingatiwa Basi Sharti Wanafunzi Wengine Wasome Chini Ya Miti.

Mwaka Jana Aliyekua Mkurugenzi Mkuu Wa Wizara Ya Elimu Katika Kaunti Ya Marsabit Paul Mwongera Alisema Kuwa Bodi Ya Elimu Katika Kaunti Hii Ilishaweka Mikakati Kabambe  Ya Kupambana Na Janga La Korona Wakati Wanafunzi Watarudi Shuleni.

Alisema Kuwa Wizara Hiyo Ilishapata Shilingi Milioni 26 Ya Kufanikisha Hilo Jambo Ambalo Kufikia Sasa Linasalia Kuwa Ndoto Kulingana Na Kilio Cha Walimu Wa Shule Za Umma.

Hayo Yanajiri Huku Chama Cha Wazazi Katika Kaunti Ya Isiolo Kikisema Kuwa Kimeridhishwa Na Ufunguzi Wa Shule Kwani Watoto Wao Walikuwa Hatarini Wakiwa Nyumbani Ikilinganishwa Na Wanapokuwa Shuleni. Ismail Ali Ni Mwenyekiti Wa Chama Cha Wazazi Kaunti Ya Isiolo Anayesema Kuwa Asilimia 82 Ya Wanafunzi Kauti Ya Isiolo Imeripoti Shuleni.

 

Subscribe to eNewsletter