Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Samuel Kosgei.
Hofu Ilitanda Jumanne Katika Eneo La Hellu Kaunti Ndogo Ya Moyale Baada Ya Kundi La Nzige Wa Jangwani Kuonekana Wakipaa Katika Eneo Hilo.
Akizungumza Na Shajara Ya Jangwani Kwa Njia Ya Simu Naibu Mkurugenzi Wa Idara Ya Kilimo Kaunti Ya Marsabit Na Pia Mkufunzi Wa Masuala Ya Nzige Hassan Charfi, Alidhibitisha Taarifa Hiyo Ila Amesema Wadudu Hao Hawakutua Eneo Hilo Na Badala Yake Walipaa Kuelekea Taifa Jirani La Ethiopia.
Charfi, Hata Hivyo Alitoa Taadhari Kwa Wakaazi Wa Kaunti Nzima Ya Marsabit Kuwa Makini Na Kuripoti Endapo Watawaona Wadudu Hao Akitaja Kuwa Wimbi La Pili La Nzige Hao Wameanza Kuwasili Jimbo Hili.
Aidha Alionya Wananchi Dhidi Ya Kufukuza Nzige Hao Wa Jangwani Kwa Njia Ya Kupiga Mayowe Au Honi Akisema Kuwa Hatua Hiyo Ya Zamani Haitasaidia Na Badala Yake Inaongeza Hali Ya Wadudu Hao Kusambaa.
Hata Hivyo, Kwa Mujibu Wa Wakazi Wa Moyale Ambao Walizungumza Na Idhaa Hii Kupitia Kipindi Cha Barizi Leo Jioni, Mamilioni Ya Nzige Hao Wameonekana Tena Katika Maeneo Ya Butiye, Manyatta Na Hellu Mjini Moyale Japo Hawajafanya Uharibifu Wowote Hadi Sasa.
Wakaazi Hao Wanaitaka Serikali Kufanya Kila Juhudi Kukabiliana Na Wadudu Hao Kabla Uharibifu Wa Maeneo Ya Malisho Na Mimea Kufanywa.