County Updates

Jeshi La Nzige Laonekana Lokesheni Ya Walda Eneo Bunge La Moyale Na Kusababisha Hofu Kwa Wenyeji.

Picha; Hisani

Na Adano Sharawe

Jeshi La Nzige Limeonekana Lokesheni Ya Walda Eneo Bunge La Moyale Na Kusababisha Hofu Kwa Wenyeji.

Kwa Mujibu Wa Chifu Wa Lokesheni Ya Walda Hassan Jattani Kotote Amesema Nzige Walionekana Eneo Hilo Jumatano Mchana Kabla Kuelekea Nchini Ethiopia Jioni.

Jattani Amesema Kundi La Nzige Hao Lilivuka Mpaka Na Kuingia Eneo La Walda Kupitia Sololo.

Vile Vile, Jattani Amesema Wenyeji Walitumia Mbinu Za Kienyeji Kama Vile Kupiga Mayowe Kuwashtua Wadudu Hao Ili Watoke Katika Mashamba Yao.

Amesema Nzige Hao Walionekana Wakila Mimea Ambayo Hutegemewa Kwa Lishe Ya Mifugo Na Wameharibu Hekta Kadhaa Za Mimea Na Kusababisha Hofu Ya Upungufu Wa Chakula Eneo Hilo.

Jattani Ameongeza Kuwa Japo Kundi Kubwa Limeondoka Eneo Hilo, Kuna Hofu Kwamba Huenda Wakarejea Na Ametoa Wito Kwa Wenyeji Kupiga Ripoti Mara Moja Endapo Watakumbana Na Nzige.

Vile Vile Amepongeza Serikali Ya Kaunti Kwa Kutuma Usaidizi Wa Haraka Na Kuchukulia Swala Hilo Kwa Uzito Unaofaa.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter