Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
NA JB NATELENG
Wito umetolewa kwa idara ya ardhi jimboni Marsabit kuweza kuwapa wakazi wa eneo la Moyale hatimiliki “title deeds” ya ardhi ili kurasmisha umiliki wa ardhi na kurahisisha kazi ya manispaa.
Wakizungumza kwenye hafla ya kuzindua manispaa ya Moyale, wakilishi wadi wa Marsabit wakiongozwa na mwakilishi wadi mteule Jillo Kiya wamesema kuwa ili kuipa manispaa ya Moyale uhuru ni sharti kila mkazi awe na stakabadhi ya kumiliki ardhi.
Wameelezea kuwa uhuru huu wa Manispaa pia utasaidia eneo hilo kupata fedha ambazo zitawanufaisha na kuwajenga kimaendeleo.
Kwa upande wake mwakilishi wadi mteule Sadia Araru ameitaka serakali ya kaunti kupitia idara ya ardhi kuweza kuhakikisha kuwa ardhi zilizonyakuliwa katika eneo la Moyale zimechukuliwa na kuwekwa chini ya umiliki wa Manispaa.