Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Waziri wa afya katika kaunti ya Marsabit Malicha Boru amekariri kujitolea kwa idara hiyo kukabiliana na ugonjwa wa Kalazaar hapa jimboni.
Akizungumza na Shajara na Radio Jangwani kwa njia ya simu,waziri Malicha amesema kwamba idara hiyo inaweka mikakati ya kunyunyizia dawa maeneo ambayo wadudu wanaoeneza ugonjwa huo wapo.
Japo ameahidi kutoa mwelekeo zaidi hapo kesho waziri huyo wa afya ametaja kwamba kwa sasa idara hiyo inaufahamu wa visa vya ugojnwa huo, jambo linaloshugulikiwa kwa sasa.