Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
NA ISAAC WAIHENYA,
Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wameonya dhidi ya kutumia njia mbadala za kusuluhisha kesi nje ya mahakama kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia.
Onyo hii limetolewa na waziri wa jinsia katika kauti ya Marsabit Jeremiah Ledanyi.
Akizungumza wakati wa zoezi lililoyaleta pamoja mashirika ya kijamii,maafisa wa serekali pamoja na washikadu wengine katika idara ya jinsia chini ya mradi wa Amkeni Wakenya,kutoka shirika la Caritas Marsabit, waziri Ledanyi ametaja kuwa kesi za dhulma za kijinsia sio moja ya kesi zinaweza kusuluhishwa kupitia mfumo huo wa AJS maarufu Alternative Justice System.
Aidha waziri Ledanyi amesema kuwa kwa sasa idara ya jinsia itahakikisha kwamba inashirikiana mashirika ya kijamii ili kufikisha hamasa kuhusiana na dhulma za kijinsia vijijini.
Waziri Ledanyi vilevile pia ameweka wazi kuwa watahusisha wanajamii ambao wamo kwenye mstari wa mbele kukemea dhulma za kijinsia kuwa mabalozi mashinani ili kuhakikisha kwamba hamasa inafika mashinani.
Hata hivyo waziri Ledanyi amelaani visa vya ufisadi vinavyotekelezwa na maafisa wa afya au wajinsia amabao wamejukumishwa kushughulikia visa vya dhulma za kijinsia akisema kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.