Wakaazi wa Karare, wanufaika na msaada wa chakula na vifaa vingine vya matumizi kutoka kwa katibu Kello Harsama.
January 9, 2025
Viongozi wa vijana viungani mwa mji wa Laisamis kaunti ya Marsabit wameonya wazee walio na hulka ya kuuza ardhi ya familia ovyo ovyo kwa bei ya kutupa.
Vijana hao kutoka eneo la Manyatta Secondary wakiongozwa na kiongozi wao Mwl. Lito Herkena ameambia shajara kuwa kuna baadhi ya wazee katika eneo hilo ambao wanauza ardhi ya jamii bila kushauriana na familia.
Zaidi ya hayo anadai kuwa wanaouza vipande hivyo vya ardhi hawana sababu mwafaka au dharura ya kuuza ardhi hizo.
Aidha amesema kuwa baadhi ya wazee wamewaunga mkono na kuahidi kushirikiana nao ili kukomesha wazee wanaouza ardhi ya familia kiholela.
Lito anasema hawana tatizo na mtu kuuza ardhi yake ila ni vyema kufuata hatua mwafaka isiyodhulumu muuzaji kwa bei.
Mzee Lodisoi Galkena kutoka eneo hilo la Laisamis ameambia shajara kuwa ni makosa kwa baadhi ya wazee kuuza ardhi ya jamii bila kuwepo kwa hitaji kubwa linalowalemea.
Anasema ardhi hizo ndizo rasilmali za jamii na zitawafaa kizazi kijacho siku za usoni.
Mzee Galkena ametishia kuwa watakaokiuka makubaliano ya kutouza ardhi ya jamii ya jamii kiholela watashtakiwa kwani tatizo likijiri katika jamii linafaa kujadiliwa ili kusaka suluhu mbadala badala ya kuuza shamba.