Local Bulletins

Wazazi wa shule ya msingi ya Bakaka,North horr, walalamikia ukosefu wa madarasa ya gredi ya tisa

Mwenyekiti wa bodi ya shule ya msingi ya Bakaka iliyoko eneo la Hurii hills eneo bunge la North horr Ibrae Sharamo amelalamikia kile amekitaja kwamba ni ukosefu wa madarasa ya gredi ya tisa.

Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Sharamo ametaja kwamba hadi kufikia sasa wanafunzi 17 wa gredi ya tisa katika shule hiyo hawajaripoti shuleni kutokana na ukosefu wa madarasa licha ya shule kufunguliwa hiyo jana wa muhula wa kwanza wa mwaka 2024.

Hata hivyo mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit, Peter Magiri kwenye mazungumzo na meza ya habari ya Radio Jangwani kupitia njia ya simu amefafanua kuwa shule hiyo ya Bakaka ni moja ya shule ambazo zimeorodheshwa katika mkumbo wa tatu na wanne kwani zinanafasi ya wanafunzi wa gredi ya tisa kuendelea na masomo kabla ya madarasa kukamilika.

Magiri amewataka wazazi kuwasialana na walimu wakuu wa shule ili kufahamu zaidi kuhusiana na hali ya gredi ya tisa kwani walimu wanauelewa kuhusiana mfumo uliotumika na kwa nini.

Kuhusiana na swala la kuchelewa kwa vitabu vya kusoma vya gredi ya 9 Magiri pia amewataka wazazi kuwa na subira kwani zoezi hilo linaendelea japo kwa mwendo wa upole.

Subscribe to eNewsletter