Local Bulletins

Wazazi Marsabit watakiwa kudhibiti matumizi ya mtandao kwa  watoto wadogo.

Na Sabalua Moses

Msimamizi mkuu  anayesimamia maswala ya watoto katika kaunti ya marsabit Mukanzi Leakey ametoa himizo kwa wazazi  pamoja na washikadau katika kaunti  ya marsabit kuwa makinifu katika kutoa udhibiti  kwa watoto wao wanapotumia mitandao ya kijamii.

Leakey  amesema ijapokua  wakaazi katika sehemu nyingi katika kaunti ya Marsabit bado hawana simu za rununu za kuingia kwenye mitandao bado kuna hatari ya watoto kujihusisha katika mambo ya ngono na ulanguzi wa watoto wanapotumia mitandao ya kijamii.

Vile vile Mukanzi amesema kuwa kuna hatari ya watoto kutumia  mitandao  bila udhibiti  na kwa sasa amewahimiza washikadau  mbali mbali pamoja na jamii kushirikiana pamoja kuripoti visa ambavyo  vinahatarisha watoto katika mitandao kaunti ya  Marsabit .

Pia amesema ni sharti washikadau wote katika kaunti ya Marsabit  washirikiane kwa pamoja ili kutoa udhibiti mwafaka kwani watoto wapo katika hatari ya ulanguzi .

Subscribe to eNewsletter