Local Bulletins

Wanaonufaika na mpango wa INUA JAMII kaunti ya Marsabit watakiwa kuwa na subira serekali inaposuluhisha baadhi ya changamoto….

Na Isaac Waihenya,

Wakaazi wanaonufaika na mpango wa serekali wa INUA JAMII katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwa na subira na kuipa serekali muda kusuluhisha baadhi ya changamo ambazo zimeukomba mfumo mpya wa kuwapa fedha zao.

Kwa mujibu afisa anyeimamia huduma za jamii katika kaunti ndogo ya Saku, Lelo Bonaya ni kuwa mfumo huo wa kuwapa fedha wanaonufaika na mpango huo ambao ni Wakongwe, Manyatima pamoja na watu wanaoishi na ulemavu umekumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo wanaonufaika kosefu wa namba za simu.

Katika mfumo huo wanaonufaika hawatakuwa wakipata fedha zao katika benki kama ilivyokuwa hapo awali bali watakuwa wakitumiwa kwa simu zao.

Aidha Bi. Lelo amewataka wanaonufaika na mpango huo kutembelea ofisi ya chifu ili kuweza kusaidika iwapo watakumbwo na changamoto zozote.

Hata hivyo Bi. Lelo amewataka wananchi kukumbatia mfumo huu mpya kwani ni bora ukilingalishwa na mifumo ya hapo awali ambayo iliwalazimu watu kusafiri mbali ili kupata fedha zao.

Subscribe to eNewsletter