Wazazi marsabit waombwa kuruhusu watoto wao kujiunga na chama cha skauti.
February 13, 2025
Na Caroline Waforo
Huku taifa likiadhimisha siku ya Redio ulimwengu leo Alhamisi chini ya kauli mbiu Redio na mabadiliko ya Tabianchi wanahabari katika kaunti ya Marsabit na kote nchini wametakiwa kutumia redio katika kuelimisha jamii jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya simu Mratibu wa Baraza la vyombo vya habari nchini MCK eneo la Kati na Mashariki mwa nchi Jackson Karanja amewataka wanahabari vilevile kutumia lugha za asilia katika kuangazia suluhu ya mabadiliko ya tabianchi kando na kuangazia athari zake.
Na huku kaunti ya Marsabit ikiwa moja wepo wa kaunti ambazo huathirika sana na mabadiliko ya hewa mratibu huyu wa vyombo vya habari amewataka wananchi kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko hayo.
Siku ya redio ulimwenguni huadhimishwa tarehe 13 mwezi februari kila mwaka ambapo redio huenziwa kwa jukumu lake la mawasiliano.
Siku hii ilitengwa pia kwa ajili ya kukuza uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa habari na kukuza maelewano kati ya jamii tofauti.
Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) lilitenga rasmi siku hii ya redio mwaka 2011.