Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
WANAFUNZI 19 kati ya 20 kutoka shule ya upili ya Ngurnit iliyo eneobunge la Laisamis watajiunga na vyuo vikuu kutokana na wao kujizolea alama ya C+ kwenda juu.
Kulingana na matokeo ya shule hiyo ni kuwa wanafunzi 8 walipata alama ya B (plain), sita walipata B-, watano wakipata C+ na mmoja akipata alama ya C. Alama wastani ya shule hIyo kwenye mtihani wa 2024 ukiwa 8.05.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Zachary Ntirgam ni kuwa hiyo ongezeko la pointi 1.65 kutoka alama wastani ya 6.4 ya mwaka wa 2023.
Katika shule ya kutwa ya Russo Mixed iliyo eneobunge la North Horr wanafunzi wawili wamepata alama ya B plain, wanane B-, Tisa C+, kumi na mmoja C plain na 6 C-.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Abduba Jaldesa ameambia jangwani kuwa shule hiyo imefanya vyema mwaka jana ikilinganishwa na mwaka wa 2023.
Shule ya Sekondari ya North imeripotiwa kupunguza alama mwaka 2024 ikilinganishwa na mwaka 2023. Kulingana na mwalimu mkuu wa shule hiyo Kuli Kofo wanafunzi wake wamejaribu kwa kupata alama wastani ya 5.2 licha idadi ndogo ya watahiniwa mwaka jana.
Katika shule ya upili ya Sassura Girls hapa Saku wanafunzi 37 wamefaulu kupata alama ya kujiunga na chuo kikuu Huku 9 wakipata alama ya kujiunga na vyuo ya kiufundi. Alama ya wastani ikiwa 6.90