Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Wanachama wa chama cha akiba na mikopo cha Rangelands Sacco chini ya shirika lisilo la kiserikali la NRT wamepata faida ukipenda dividends ya shilingi milioni 6 baada ya kuwekeza katika chama hicho.
Mwanachama aliyepata dividends za juu zaidi akipata zaidi ya shilingi 200,000.
Haya yalibainika Jumanne wakati wa mkutano wa kila mwaka wa wajumbe wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Archers Post town, kaunti ya Samburu.
Akizungumza na wahabari afisa mkuu wa kitengo cha biashara katika Rangelands Sacco Peter Nguno amesema kuwa chama hicho kinawafaidi wananchi kutoka kaunti za wafugaji ili kujitegemea kwa kuwekeza katika biashara.
Nguno anasema kuwa wanawawezesha wanachama wa chama hicho cha akiba ili nao wawezeshe jamii kukabiliana na changamoto ambazo hushudiwa katika kaunti za wafugaji.
Na ni katika mkutano huo ambapo wanachama mbalimbali walituzwa wakiwemo wanachama waliokopo na kurejesha