Local Bulletins

Wanabodaboda, Marsabit wakosoa mswaada wa sheria za bodaboda.

Na Joseph Muchai,

Wanabodaboda katika mjini Marsabit wamekosoa mswada unaohusu kubadilishwa kwa sheria za bodaboda humu nchini.

Baadhi ya waliosema na idhaa hii wametaja kuwa mswaada huo ulitungwa kinyume cha sheria kwani wao hawakuhusishwa ili kutoa maoni yao kabla ya mswada huo kubuniwa.

Aidha wanabodaboda hao wanasema kuwa ni usaliti mkubwa kwani serikali ya Kenya Kwanza iliwaahidi wanabodaboda na wanabiashara nchini kuwa maisha yao yangeinuliwa viwango swala ambalo kwa sasa limesalia kuwa ndoto.

Kwa sasa wanakiri kuwa wanaendelea kuhangaika kutokana na gharama ya juu ya maisha ilihali serikali inaonekana kuyafumbia macho madhila ya wananchi. Mswada huo uliwasilishwa kwenye bunge la seneti na seneta wa Kakamega Bonny Khalwale.

Baadhi ya maswala yanayopendekezwa katika mswaada huo ni ikiwemo sharti la kuvalia kofia za pikipiki kwa waendeshaji bodaboda na mteja wake, kubeba mizigo isiyozidi kilo hamsini miongoni mwa maswala mengine

Subscribe to eNewsletter