Local Bulletins

Wakulima jimboni Marsabit watakiwa kuchukua tahathari ya kiangazi kati ya mwezi machi na mei mwaka huu…

Na Joseph Muchai,

Wakulima na wafugaji katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuchukua tahadhari na kujiandaa kwa usalama wa chakula siku za hivi karibuni.

Hii ni baada ya tahadhari kutolewa na idara la utabiri wa hali ya hewa humu nchini kuonya kuwa kutashuhudiwa uhaba wa mvua kati ya mwezi Machi Aprili na Mei mwaka huu wa 2025.

Akiongea na kituo hichi ofisini mwake,afisaa mkuu wa kilimo katika kaunti ndogo ya Saku kaunti ya Marsabit Duba Nura ameonya kuwa ni vyema kwa wakulima kutuamia vyakula kwa uwajibikaji kwani uhaba wa chakula umeanza kushuhudiwa katika baadhi ya maeneo kaunti ya Marsabit.

Kulingana na Nura lishe ya mifugo kwa sasa imepungua kutokana na kiangazi kinachoshuhudiwa katika maeneo mbali mbali hapa jimboni huku akionya kuwa hali hiyo huendea ikawa mbaya zaidi siku za usoni.

 Wakati uo huo Nura amewasihi wafugaji kuuza mifugo wao kabla ya athari kutokea.

Kulingana na afisa huyo kwa sasa hakuna lishe ya kutosha kwa mifugo hilo likimaanisha kuwa huenda mifugo wengi wakadhoofika kuotokana na uhaba wa lishe na maji.

Haya yanajiri huku idara ya hali ya hewa ya nchini ikinatabiri hali ya Joto, Ukavu, na jua kote nchini, na joto la mchana linaongezeka zaidi ya nyuji joto 30 ° C katika maeneo mengi ya nchi.

Hata hivyo maeneo la kati mwa nchi, kusini mwa bonde la Ufa la Kusini, na vyungani vya Ziwa la Victoria yatashuhudia viwango vya joto vya chini ya nyuzi joto 30 ° C.

Joto la wakati wa usiku katika nyanda za juu mashariki mwa bonde la ufa linaweza kushuka chini ya nyuzi joto 10 ° C.

Pia mvua chache inatarajiwa katika maeneo machache, haswa karibu na Mlima Kenya, eneo la Pwani, na sehemu za Ziwa Victoria.

Subscribe to eNewsletter