Local Bulletins

Wakristo jimboni Marsabit watakiwa kumuombea Papa mtakatifu Francisco ambaye anaendelea na matibabu.

Wakristo jimboni Marsabit watakiwa kumuombea Papa mtakatifu Francisco ambaye anaendelea na matibabu.

Na JB Nateleng,

Wito umetolewa kwa Wakristo kumuombea Papa mtakatifu Francisco ambaye anaendelea na matibabu.

Kwa mujibu wa baba wa paroko wa Kathedrali ya Marsabit Padri Tito Makokha ni kuwa Wakristo wanafaa kumuombea Papa mtakatifu Francisco ambaye amekuwa akipokea matibabu kwa muda wa wiki moja sasa.

Padri Tito amewataka Wakristo jimboni Marsabit kutenga muda na kusali Rosari takatifu na pia kushiriki misa takatifu kwa ajili ya afya ya Papa mtakatifu Francisco ili Mungu mwenyezi ampe afya njema na kumfanya aendelee kuhudumia kanisa.

Aidha Padri Tito ameungana na Maaskofu nchini Kenya ambao walikuwa wametoa wito wa kumuombea Papa mtakatifu.

Na huku wanafunzi wakianza likizo fupi wiki hii, Padri Tito amesema kuwa ni sharti wanafunzi wadumu katika sala siku zote na kuwasaidia wazazi nyumbani kwani hilo liwaepusha na madhara katika jamii.

Subscribe to eNewsletter