Local Bulletins

Wakazi wa vijiji vya Nawapa,Kulamawe na Kilimambogo Loiyangalani,wamelalamikia uhaba wa maji…

Na JB Nateleng,

Wakazi wa vijiji vya Nawapa, Kulamawe na Kilimambogo eneo la Loiyangalani, eneo Bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit wamelalamikia uhaba wa maji na kuitaka idara ya maji kuingilia kati na kutatua changamoto hiyo.

Wakizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, wakazi hao wamesema kuwa wamekumbwa na changamoto ya maji kwa kipindi cha miaka miwili sasa jambo ambalo linaloadhiri usafi na hata maswala ya afya yao.

 kwa sababu wanasafiri masafa marefu kusaka maji ambayo hata wakati mwingine huwa wanankosa na kuerejea nyumbani bila Maji.

Wamesema kuwa uhaba huo wa maji katika vijiji hivi pia unaathiri masomo ya watoto kwa sababu watoto huwa wanachukua muda mrefu kuenda kuteka maji hivyo kuwafanya kuchelewa kufika shuleni na hata muda mwingine kukosa kuhudhuria masomo.

Wameitaka serekali kuingilia kati na kuhakikisha kwamba wanapata bidhaa hiyo muhimu kama vijiji vingine katika eneo hilo.

Kwa upande wa wasimamizi wa wahudumu wa afya wa nyanjani CHPs katika vijiji hivyo, wakiongozwa na Ziporosa Akiru pamoja na Caroline Emuron ni kuwa pia imekuwa changamoto kwao kuweza kufunza kuhusu usafi wa mazingira kwa sababu ya uhaba wa maji katika vijiji hivyo na kurai serekali kuweza kuwahakikishia upatikanaji wa maji kwa manufaa ya wakazi hao.

Subscribe to eNewsletter