Idara ya maji Marsabit yaahidi kukabiliana na utata unaozunguka kero la maji
January 20, 2025
Siku chache tu baada ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta kuwahimiza vijana wa Kenya kupigania haki wakazi wa mji wa Marsabit wameunga mkono matamshi yake wakisema kuwa yanatia moyo wananchi kusimama imara na kupigani haki yao.
Baadhi ya waliozungumza na idhaa hii wamesema kuwa, matamshi yake Uhuru Kenyatta yanadhihirisha kuwa serekali ya sasa ina mapengo mengi ambayo yanafaa kusuluhishwa na wananchi ambao waliwachagua.
Wamesisitiza kuwa watasimama imara katika kuwashinikiza viongozi kuwajibika kwa kuwaletea maendeleo mashinani kwa sababu hiyo ndio lengo kuu la wao kuchaguliwa.
Hata hivyo wamewakashifu viongozi wa kisiasa ambao wanahisi kuwa wamekerwa na maneno ya Uhuru wakisema kuwa ni muda wao kukaza Kamba katika kuwafanyia wakenya kazi.
Itakumbukwa kuwa wiki jana, Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alitoa matamshi yanayofasiriwa kama kuunga mkono maandamano ya vijana nchini kwa kuwahimiza kujitokeza kupigania haki zao.
Rais William Ruto siku ya Jumapili akizungumza kaunti ya Bungoma alionekana kumjibu rais mstaafu Uhuru akimtaka kukoma kuchochea vijana kupitia ghasia kama yaliyoshuhudiwa mwezi Juni mwaka jana wakati wa maandamano ya kizazi cha Gen Z