Local Bulletins

Wakaazi wa mji wa Marsabit watoa maoni mseto kuhusu ada ya kujisajili kuchua kitambulisho cha kitaifa.

Na Joseph Muchai

Siku moja baada ya kiongozi wa chama cha NARC Kenya Martha karua kukosoa serikali kwa kulipiza ada ya shilingi elfu moja mtu anaposajiliwa kuchukua kitambulisho cha kitaifa kwa mara ya kwanza wakaazi wametoa maoni yao kuhusiana na swala hilo. Baadhi yao wanahoji kuwa serikali ina nia ya kuwafungia vijana kupata nafasi za kazi na pia katika shughuli ya uchaguzi.

Hiyo jana karua alidai kuwa serikali ina lengo la kuwafungia vijana nje ya zoezi la uchaguzi hivyo basi kuwanyima haki ya kikatiba.

Itakumbukwa kuwa serikali ilipitisha sheria ya kutoza shilingi elfu moja kwa mtu anayejisajili kwa mara ya kwanza na shilingi 2000 kwa mtu anayetafuta kitambulisho baada ya kupoteza.

Wakati uo huo… Baadhi ya wakaazi mjini Marsabit wametoa maoni ya wakikosoa kauli ya serikali kuhusiana na kushuka kwa gharama ya maisha nchini. Wakiongea na idhaa hii wakaazi wamesema kuwa gharama ya maisha imezidi kupanda haswa kutokana na ukosefu wa ajira.

Subscribe to eNewsletter