Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Na Samuel Kosgei
Baadhi ya wakazi wa wadi ya Marsabit Central mjini Marsabit wametaja kusikistishwa na hatua ya idara ya fedha kaunti ya Marsabit kuahirisha vikao vya kitoa maoni yaliyopangwa kufanyika Alhamisi katika ofisi ya chifu wa Lokesheni Ya Mountain.
Wakaazi hao wakiongozwa na Dokata Kuro ambaye ni kiongozi wa watu wanaoishi na ulemavu amesema kuwa inasikitisha kuona kuwa vikao hivyo viliahirishwa ghafla bila wao kujulishwa na idara inayohusika.
Baadhi yao pia wanasema kuwa idara husika ingetoa tangazo la kuahirishwa kwa vikao hivyo kupitia vyombo vya habari za marsabit ili kuendana na wakati wao kwani wanahisi kuharibiwa muda wao mwingi.
Mohamed Hassan ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya kijamii mjini marsabit amesema ni makossa kwa idara husika kuahirisha vikao hivyo bila ufahamu wa umma kupitia njia hitajika.
Amemtaka gavana wa kaunti ya Marsabit kuhakikisha idara husika kwenye masuala yanayohusu mwananchi zinawajibishwa kwa kutelekeza mahitaji ya wananchi.
Mratibu wa wadi ya Central Abdub Isako ameambia shajara kuwa mkutano huo uliahirishwa hadi siku ya Ijumaa kutokana na kuchelewa kwa mawasiliano kutoka idara ya fedha. Amedai kuwa hakufahamu kuhusu mkutano huo na alijulishwa katika dakika za mwisho siku Jumatano.