Local Bulletins

Wakaazi wa Marsabit kuasi kukata miti na kuchoma makaa ili kuzuia uharibifu wa mazingira….

NA ISAAC WAIHENYA

 Wito umetolewa kwa wakaazi wa Marsabit kuasi kukata miti na kuchoma makaa ili kuzuia uharibifu zaidi wa mazingira.

Kwa mujibu wa mshirikikishi wa maswala ya kawi katika kaunti ya Marsabit Joseph Agola ni kuwa jamii inafaa kuwa makini na matumizi ya makaa na kuni ili kuzuia uharibifu zaidi wa mazingira unaosababisha mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani ofisini mwake Agola ametaja kwamba ipo hoja ya jamii ya Marsabit kukumbatia mbinu mbadala ya upishi kama vile jiko za kisasa ambazo haziharibu mazingira kwa kiwango kikubwa.

Aidha Agola amesema kuwa licha ya kaunti ya Marsabit kuwa na idadi kubwa ya mifugo, Agola ametaja kwamba itakuwa vigumu kwa mfumo wa kawi wa Biogas kufaulu kutokana na zoezi la wafugaji kuhamahama.

Kadhalika Agola ametoa wito kwa jamii kupanda miti na kutunza iliyopo ili kuepusha uharibifu zaidi wa mazingira.

 

 

 

 

 

Subscribe to eNewsletter