Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Na Samuel Kosgei
Wananchi wanaoishi katika lokesheni ya Mountain wadi ya Marsabit Central eneobunge la Saku wameonesha masikitiko yao kutokana na kutopewa stakabadhi ya kumiliki ardhi (tittle deeds) mwezi wa tisa mwaka jana kama walivyokuwa wameahidiwa na viongozi wao wakiongozwa na MCA wa eneo hilo.
Wakazi hao wakiongozwa na mwanaharakati wa haki za kibinadamu Mohammed Hassan kutoka shirika la Centre for Research, Rights and Development (CRRD) wamesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita wao kama wananchi wamekuwa wakitenga pesa kwa ajili ya kupata tittle deeds kwenye vikao vya kutoa maoni lakini kufikia sasa imesalia kuwa ndoto kwani hilo halijatimia.
Hassan amedai kuwa mwaka kifedha wa 2024/25 wakaazi wa eneo la Wabera Grading Scheme walitenga shilingi milioni 8 kwa ajili za kusaidia kutoa tittle deeds.
Hassan pia alitaka kujua jinsi pesa za miradi ya maji ilivyotumika licha ya kuwepo kwa bajeti, kwani kufikia sasa serikali ya kaunti imepokea usaidizi wa kuweka mabomba ya maji mjini Marsabit.
Ameshutuma wawakilishi wadi wa Marsabit kwa kutofuatilia miradi iliyopendekezwa na wananchi wakati wa vikao vya kutoa maoni nyingi akisema inabadilishwa na wao wenyewe.
Wakati uo Hassan amepinga ripoti ya mdhibiti wa bajeti iliyodai kuwa Marsabit inaongoza kote nchini kwa kutenga pesa za maendeleo akidai kuwa maendeleo yenyewe hayaonekani.