Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
NA ISAAC WAIHENYA
Wakaazi wa eneo la Kambinye wameishukuru irada ya maeneo kame inayoongozwa na katibu wa maeneo kame na maendeleo ya miji Kello Harsama kwa kila wamekitaja kwamba ni kuwajali katika kipindi hichi cha ukame.
Wakizungumza na Shajara ya Radio Jangwani, wakaazi hao wametaja kwamba wamepokea chakula hiocho ambacho kitawasukumu kwa majumaa kadhaa na kuwaepusha na baa la njaa.
Aidha baadhi yao kutoka maeneo ambayo hayajapata chakula wamemtaka katibu Kello Harsama kuhakikisha kwamba wao pia wanapata huku wakishukuru katibu huyo kwa kufanikisha miradi mbalimbali katika eneo hilo.
Kauli zao zilishabikiwa na wakaazi wa eneo la Korr ambao wamedhibitisha kupokea chakula kutoka kwa katibu Kello Hrasama siku chache zilizopita wakitaja kwamba kiligawanywa kwa njia inayofaa kwa wananchi wa eneo hilo.