Viongozi Marsabit wakosoa hatua ya serekali kuvunjilia mbali shirika la NACONNET….
February 4, 2025
NA ABDILAZIZ ABDI
Wakaazi wa kata ya Golole wadi ya Uran kataika emneo bunge la Moyale wanalalamikia kile wanachokidai kuwa ni ukosefu wa mtandao
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, wamesema kuwa ukosefu wa mtandao umeduwaza mawasiliano baina yao na watu wengine.
Aidha wamesema swala hilo limepelekea wao kubaki nyuma kimaendeleo.
Vilevile wakazi hao wametaja ukosefu wa mtandao katika eneo hilo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa ajaira hasa miongoni mwa vijana wanaotegemea fursa kuputia mitandao.
Wengine wao wametoa wito kwa serikali ya kaunti na mamlaka ya mawasiliano kuchukua hatua ya darura kuimarisha huduma hiyo.