Wakaazi wa Karare, wanufaika na msaada wa chakula na vifaa vingine vya matumizi kutoka kwa katibu Kello Harsama.
January 9, 2025
Wakaazi wa eneo la Karare,eneo bunge la Saku, kaunti ya Marsabit wamenufaika na msaada wa chakula na vifaa vingine vya matumizi kutoka kwa katibu wa maeneo kame na maendeleo ya mikoa nchini Kello Harsama.
Msaada huo unajumuisha vyakula, blanketi pamoja na taulo za kutumiwa na wanawake na wasichana wakati wa hedhi.
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya kupokea msaada huo, MCA wa wadi ya Karare Joseph Leruk amewarai viongozi mbalimbali serekalini kuhakikisha kwamaba wanawapa msaada wanajamii haswa wa chakula kipindi hichi cha kiangazi.
Aidha baadhi ya wananchi walionufaika na msaada huo wakiongozwa na Antonella Serelek na mzee Joseph Lemorogo wamempongeza katibu Kello kwa kuwakumbuka kwani bado wananchi wa eneo hilo wanakubwa na njaa.