Local Bulletins

Wakaazi wa Karare scheme walalamikia uhaba wa maji na kuhangaishwa na ndovu

Wakaazi wa Karare Kaunti ya Marsabit wamelalamikia uhaba wa maji katika maeneo hayo.  Kulingana nao ni hali ambayo imesalia kuwa donda sugu kutokana na kuharibiwa kwa mifereji ya maji na ndovu.

Sasa wakaazi wanaomba shirika la huduma za wanyamapori kuingilia kati na kuwazuia ndovu kufanya uharibifu.

Chifu wa eneo hilo Magdalena Ilimo ameomba serikali kusaidia kuwatatulia tatizo hilo akisema akina mama wa maeneo hayo wamekiwa wakitembea masafa marefu kutafuta bidhaa hiyo muhimu.

Wakati uo huo wakaazi wamesema kuwa wanaishi kwa hofu kutokana na hatari ya kushambuliwa na wanyama hao hatari.

Mwenyekiti wa Bongole Water Users Mike Nepe hata hivyo ameeleza kuwa kuna matumaini kwani ujenzi wa mifereji ya maji inafanyiwa marekebisho. Aidha anaomba KWS kuingilia Kati na kufanya wajibu wao.

Wakati uo huo… Wakazi hao wamelalamikia kubaguliwa katika nafasi za ajira ya polisi wa akiba NPR. Wakiongea wakati wa kikao cha uhamasishaji kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha teknolojia ICT centre katika eneo hilo kilichohudhuiwa na naibu wa kamishna wa kaunti ya Marsabit David Saruni wakaazi hao wanasema kuwa idadi ya nafasi waliopewa haiendani na ukubwa wa dadi ya wakaazi.

 Wakati uohuo wakaazi hao wanadai kuhangaika wakati wa usajili wa vitambulisho sasa wakiomba serikali kulingilia kati na kuwaletea huduma katika maeneo yao  kwani kwa kipindi kirefu sasa serikali imekuwa ikiwahudumia kutoka Marsabit mjini baada ya kusitisha huduma hizo katika maeneo hayo.

Wanalalama kusafiri masafa marefu kwenye shughuli ya kutafuta huduma nyingine muhimu za serikali.

 

Subscribe to eNewsletter