Local Bulletins

Wakaazi wa eneo la Karare walalamikia ukosefu wa maji baada ya ndovu kuharibu mifereji ya maji.

Na Joseph Muchai,

Wakaazi wa eneo la Karare wanaendelea kutaabika kutokana na ufaba waji katika eneo hilo huku wakilazimika kutembea masafa marefu kutafuta bidhaa hiyo adimu.

Akiongea na kituo hiki kwa njia ya simu chifu wa eneo hilo Magdaline Ilimo ameelezea kuwa kilio chao hakijasikilizwa hata licha yao kulalama kwa muda mrefu.

Wakati uo huo Chifu Ilimo amesema kuwa wakaaazi wa eneo hilo wanalazimika kutembea hadi katika maeneo ya Bong’ole kutafuta maji ilhali maji hayo yanangewafikia iwapo idara ya wanyamapori ingechukua hatua mujarabu na kuwajengea ndovu sehemu za kunywea maji badala kuacha ndovu kuwahangaisha wakaaji punde tu wanapokamilisha urekebishaji wa mifereji ya maji.

Itakumbukwa kuwa juma lililopita wakaazi wa eneo hilo walilalama kuhangaishwa na ndovu wanaowasababishia mahangaiko. Hata hivyo tulipozungumza na maafisaa wa KWS hiyo juzi waliarifu kuwa wakaazi hao bado hawajapiga ripoti rasmi kuhusiana na tatizo hilo kwao.

Kulingana na chifu Ilimo tatizo hillo limeasalia kuwakodolea macho huku kilio chao kikiambulia pakavu.

Subscribe to eNewsletter