Wakaazi wa Marsabit wakerwa na hatua ya kuahirishwa kwa vikao vya kutoa maoni bila kujulishwa mapema.
February 20, 2025
Na Henry Khoyan,
Wakaazi jimboni Marsabit wametoa hisia zao kuhusiana na pendekezo la kumpa kinara wa ODM Raila Odinga nafasi ya Waziri Mkuu katika serikali ya Kenya Kwanza.
Wakizungumza na Radio Jangwani, baadhi ya wakaazi hao wameunga mkono pendekezo hilo wakisema kuwa litasaidia kuleta umoja na maendeleo humu nchini.
Aidha baadhi yao wameonekana kupinga pendekezo hilo wakieleza kuwa umri wa Raila Odinga umesonga na hafai tena kupewa nafasi ya Waziri Mkuu na badala yake wakamtaka astaafu kwenye siasa za kitaifa.
Wakaazi hao wameeleza kuwa kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kushikilia nafasi hiyo kando na Raila Odinga.
Pendekezo la Raila limeshika kasi huku likisukumizwa na wendani wa rais Ruto haswa baada ya Raila Odinga kupoteza nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Afrika AUC katika uchaguzi ulioandaliwa jiji Adis Ababa nchini Ethiopia jumamosi iliyopita.