Local Bulletins

Waititu apatikana na hatia katika kesi ya ufisadi ya shilingi milioni 588

NA SAMUEL KOSGEI

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu, mke wake Susan Wangari  na maafisa wawili wa kaunti,wamepatikana na hatia katika kesi ya utoaji zabuni kinyume na sheria ya shilingi milioni 588.

Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano, Hakimu Mkuu Thomas Nzioki alisema washukiwa hao walipatikana na makosa 9 kati ya 12 yaliyowasilishwa mahakamani dhidi yao.

Baadhi ya mashtaka yaliyowakabili ni pamoja na ufisadi, ukinzani wa maslahi, ulanguzi wa pesa, utumizi mbaya wa mamlaka na kujihusisha na mali ya kutiliwa shaka, miongoni mwa mengine.

Kulingana na Hakimu huyo Mkuu, upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha kwamba washukiwa hao walitekeleza makosa 9 kati ya 12 yaliyowasilishwa dhidi yao.

Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaondolea mashtaka matatu yaliyohusishwa na ulanguzi wa pesa.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya washukiwa hao baadaye leo alasiri.

Waititu na wenzake wanazuiliwa katika korokoro za polisi katika kituo cha polisi cha Milimani

 

 

Subscribe to eNewsletter