Local Bulletins

Wafugaji Narok,wahimizwa kukukubali chanjo kutolewa kwa mifugo wao….

Na Isaac Waihenya,

Naibu Gavana wa Narok, Tamalinye Koech amewahimiza wafugaji kutoka kaunti hiyo kukukubali chanjo kutolewa kwa mifugo wao akisema kwamba itakuwa ya manufaa zaidi kwani mifugo hao watalindwa dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Akizungumza na waadhishi wa habari naibu Gavana huyo amesisitiza haja ya wananachi kutopotoshwa na watu wanaolenga kuhakikisha kwamba wafugaji humu nchini hawatasaidika na wala kunufaika na ufugaji wa mifugo.

Ameweka wazi kuwa zoezi hilo limeng’oa nanga rasmi katika kaunti hiyo huku akiongeza kuwa hakuna mwananchi yeyote atakayelazimishwa kuwapa mifugo wake chanjo.

Aidha Koech amewataka viongozi pia kujitokeza kusaidia kuwaelekeza wananchi kuhusiana na umuhimu wa chanjo hiyo ili waache kuipinga bila kufahamu ni vipi itawanufaisha.

Subscribe to eNewsletter