Viongozi Marsabit wakosoa hatua ya serekali kuvunjilia mbali shirika la NACONNET….
February 4, 2025
NA JB NATELENG
Huku dunia ikiadhimisha wiki ya Maelewano ya Dini Ulimwenguni, wito umetolewa kwa viongozi wa dini kuweza kueneza injili kwa waumini bila ubaguzi huku viongozi hawa wakishauriwa kuweza kujitolea kikamilifu katika kufuata na kuendeleza uhusiano mwema kati ya madhehebu mbalimbali jimboni Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, mhubiri Saido Diba ambaye ni mwenyekiti wa muungano wa wahubiri jimboni Marsabit amesema kuwa ni wajibu wa viongozi wa kidini kuweza kuwaongoza waumini vyema na kuwashauri kuheshimu madhehebu mengine.
Diba ameelezea kuwa kumekuweko na ushirikiano baina ya Wahubiri, Mapadri, Maaskofu na Maimamu katika kaunti ya Marsabit huku akitoa wito kwa viongozi hao kuendelea vivyo hivyo kwa manufaa ya kuleta na kujenga mapatano baina ya waumini wa dini zote jimboni Marsabit.
Aidha mhubiri Diba amewataka wanasiasa pia kuasi kasumba ya kuleta siasa kanisani akisema kuwa hili litaaribu muonekano wa kanisa kama chumba cha maombi.
Kadhalika mhubiri huyu amewataka waumini wa madhehebu tofauti jimboni kuweza kuishi kwa upendo na kulihubiri neno bila kuegemea dini wala kabila.