Wasichana na wanawake Marsabit watakiwa kufanya kozi ya sayansi ili kuendana soko la ajira.
February 11, 2025
Na JB Nateleng’
Mbunge wa Saku Ali Dido Rasso ametoa wito kwa vijana katika eneo la Saku kaunti ya Marsabt kuweza kujiunga na vyuo anuwai vilivyo jimboni Marsabit.
Akizungumza katika shule ya upili ya Gadamoji alipokuwa akikabidhi shule hiyo basi pamoja na kuzindua mkatati wa miaka mitano ya shule hiyo, Rasso amewataka vijana katika eneo la Saku kuweza kukumbatia masomo ya vyuo anuwai ili kupata ujuzi ambao utawawezesha kujiboresha kimaisha.
Rasso amesisitiza umuhimu wa vyuo vya anuwai akisema kuwa serekalii inazidi kuwekeza katika vyuo hivi ili kufaidisha vijana katika jamii
Mbunge Rasso vile vile amesikitikia idadi ndogo ya Wanamarsabit ambao wamejisajili katika bima mpya ya afya ya SHA akiwataka wanaMarsabit kujitokeza na kujisajili katika bima hii ili kupata matibabu kwa bei nafuu.
Mbunge huyu amesifia utulivu ambao umesheheni katika kaunti ya Marsabit akiwahimiza wakazi kuzidi kukumbati Amani ili kuendelea kufurahia maendeleo.
Huku Rais William Ruto akitarajiwa kuzuru kaunti ya Marsabit hivi Karibuni, Mbunge Rasso amewataka wakazi wa kaunti hii kuwa watulivu na kuheshimu ujio wa Rais kwa sababu itakuwa na manufaa.