Local Bulletins

Upungufu wa maafisa wa kuhamsisha umaa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi wachangia kudorora kwa kilimo Marsabit…

Na JB Nateleng,

Kuna haja ya kutoa hamasa kwa wakulima kuhusu mbinu sahihi ya kilimo katika kaunti ya Marsabit, baada ya asilimia kubwa ya wakulima kupata hasara msimu uliopita wa mvua.

Haya ni kwa mujibu wa afisa wa kilimo katika kaunti ya Marsabit Dub Nura.

 Akizungumza kwenye hafla ya kutoa hamasa ambayo iliandaliwa katika shule ya upili ya Dibayu, eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit iliyowaleta pamoja wakulima zaidi ya 500 kutoka eneo la Saku, Dub amesema kuwa iwapo wakulima watahusishwa kikamilivu kwa masuala ya kilimo dijitali basi kutakuwepo na mavuno ya kutosha kwa sababu mbinu za kisasa ni sahihi, nafuu na rahisi kueleweka.

Dub amesisitiza ushirikiano baina ya mashirika yasiyo ya kiserekali na idara hiyo ili kufanikisha mpango wa kutoa hamasa kwa wakulima jimboni.

Aidha Dub amesema kuwa kama serekali ya kaunti wanahakikisha kuwa wamepasha habari ipasavyo ili kuwaepusha wakulima kupata hasara na kuwepo na mavuno ya kutosha msimu wa mvua na pia msimu wa kiangazi.

Afisa huyo wa kilimo ameeleza kuwa upungufu wa maafisa wa kusaidia katika kupeana habari kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unachangia katika kudorora kwa kilimo jimboni jambo ambalo amesema linafaa kuangaziwa kwa kina ili kuwepo na uhakika wa upatikanaji wa mapato ya kutosha.

Subscribe to eNewsletter