Wazazi wa shule ya upili ya Sasura girls wamkataa mwalimu mkuu mpya aliyehamishiwa shuleni humo.
January 14, 2025
Na Caroline Waforo,
Ugonjwa wa kichaa cha umbwa umerokodiwa katika eneo la Forole eneo bunge la Northhorr kaunti ya Marsabit.
Haya ni kulingana na Afisa wa kufuatilia magonjwa ya mifugo jimboni Marsabit Dkt Bernard Chege.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani daktari Chege amesema kuwa ugonjwa huo wa kichaa cha mbwa pia unashukiwa kuwepo katika eneo la Loiyangalani.
Aidha daktari Chege amedokeza kuwa ugonjwa wa Canine distemper umerekodiwa miongoni wa umbwa katika wadi ya Karare huku ukichochewa na uwepo wa mbuga ya wanyama.
Daktari Chega anasema kuwa kama idara wameweka mikakati ya kukinga wanadamu pamoja na mbwa dhidi ya ugonjwa huo wa kichaa cha mbwa.
Ugonjwa wa kichaa cha mbwa huambukizwa kwa kungatwa na mnyama aliyebeba virusi hivyo viitwavyo rabies.
Maambukizi kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu yanaweza kutokea pia iwapo mnyama mwenye virusi hivyo atagusana na kidonda kibichi cha binadamu.