Wazee waonywa dhidi ya kusuluhisha kesi za dhulma za kijinsia vijini…
January 30, 2025
NA ISAAC WAIHENYA
Wito umetolewa kwa washikadau mbalimbali wanaoshughulikia haki za watoto katika kaunti ya Marsabit kuasi ufisadi wakati wa kushughulikia kesi za dhulma za kijinsia.
Kwa mujibu wa afisa wa miradi katika mradi wa Amkeni Wakenya,kutoka shirika la Caritas Marsabit, George Galgallo ni kuwa baadhi ya waadhiriwa wa dhulma za kijinsia hapa jimboni wamekuwa wakikosa haki kutokana na uwepo wa ufisadi.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kutoa hamasa kwa mashirika ya kijamii,maafisa wa serekali pamoja na washikadu wengine katika idara ya jinsia ulioandaliwa hii leo katika eneo la Pastoral Center hapa jimboni Marsabit, Galgallo ametaja ametoa onyo kwa watakaohusika kwenye ufisadi ili kuwanyima haki waadhiriwa kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kando na hilo Galgallo ameutaja umaskini kama swala jingine ambalo linaadhiri vita dhidi ya dhulma za kijinsia hapa jimboni Marsabit.