Local Bulletins

Shirika la Child Fund kwa ushirikiano na Econic Earth lawazawadi wanafunzi wa shule ya msingi ya Bubisa taa 2,500 za sola….

Na Isaac Waihenya,

Sasa ni afueni kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Bubisa katika eneo Bubisa kaunti ya Marsabit baada ya shirika la Child Fund kwa ushirikiano na Econic Earth kuwazawadi taa 2,500 za sola zitakazowafaidi katika masomo yao.

Kwa mujibu wa mkurungezi wa shirika la Child Fund nchini Alice Kamau ni kuwa mradi huo ambao utaendeshwa na shirika la Nawiri Child development program katika kaunti ya Marsabit unalenga kuhakikisha kwamba wanafunzi kutoka eneo hili waendleza masomo yao bila kutatizika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la kusambaza taa hizo katika shule ya msingi ya Bubisa, Bi. Kamau amesema kuwa shirika la Child Fund litahalikisha kwamba haki elimu za watoto zinazingatiwa kikamilifu hapa jimboni Marsabit,huku akiwarai wazazi kuwapa watoto haki ya elimu bila masharti yeyote.

 Bi Kamau amewataka wazazi kuhakikisha kwamba taa hizo zinawanufaisha watoto katika masomo yao kabla ya kuhusika katika maswala mengine ya kinyumbani.

Kwa upade wake mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit aliyezungumza katika hafla ya leo, ameahidi kuwa idara ya elimu itashirikiana na shirika la Nawiri Child development Program kufanikisha elimu jimboni Marsabit.

Aidha Magiri amepongeza mradi huo huku akisema kuwa utafanikisha na kuboresha elimu katika kaunti ya Marsabit.

Aidha baadhi ya wanafunzi walionufaika na mradi huo wamelishukuru shirika la Child Fund huku wakitaja kwamba taa hizo za sola zitawaondolea masumbuko waliokuwanayo wakisoma nyakati za usiku.

Subscribe to eNewsletter