Local Bulletins

Serikali yazindua operesheni kali ya Ondoa Jangili katika kaunti za Marsabit na Isiolo.

Na Waandishi Wetu,

Serikali kupitia idara ya polisi nchini imezindua operesheni kali ya Ondoa Jangili katika kaunti za Marsabit na Isiolo.

Operesheni hii inalenga kuwaondoa wahalifu kutoka kundi la Oromo liberation Army {OLA} linaloaminika kuendeleza shughuli za uhalifu katika kaunti hizi mbili ikiwemo biashara ya bunduki harama na ulanguzi wa dawa za kulevya na binadamu kati ya nyinginezo kupitia mpaka wa Kenya na Ethiopia.

Haya yametangazwa na naibu Inspekta Jenerali wa polisi Gilbert Masengeli ambaye amefanya ziara ya ghafla katika kaunti ya Marsabit leo hii.

Masengeli amesema kuwa wanachama wa kundi hilo wanajificha miongoni mwa jamii katika kaunti za Marsabit na Isiolo katika kuendeleza uhalifu huu haswa kwa wananchi wanaoishi mpakani mwa Kenya na Ethiopia ikiwemo ubakaji wa wanawake.

Hata hivyo Masengeli amewawarai wananchi kushirikiana na idara ya polisi ili kufanikisha operesheni hii ya Maliza Jangili.

Na kuhusiana na migodi ya Hillo iliyoko eneo la Dabel eneo bunge la Moyale, Masengeli amesema kuwa mikakati ya kiusalama inawekwa kuhakikisha kuwa usalama utadumishwa wakati migodi itakapofunguliwa rasmi.

Subscribe to eNewsletter