Afueni kwa wanafunzi 132 wa shule ya upili ya Goro Rukesa baada ya KNEC kuachilia matokeo ya mitihani yao….
January 21, 2025
Na Samuel Kosgei
MSEMAJI wa serikali ya Marsabit Abdub Barille amewataka wazazi wa wanafunzi wanaofadhiliwa na serikali ya kaunti kutokuwa na hofu kuhusu hatima ya ufadhili huo wa kaunti kutokana na magavana kote nchini kuonywa na mdhibiti wa bajeti dhidi ya kutenga pesa za kufadhili masomo kwa wanafunzi wasiojiweza katika kaunti.
Barile amesema kuwa licha ya onyo hiyo ya mdhibiti wa bajeti Margaret Nyakango, baraza la magavana linafuatilia suala hilo kwa karibu na wana imani kuwa wanafunzi wataendelea kulipiwa elimu yao na kaunti katika viwango vya shule za sekondari, taasisi za kiufundi na hata vyuo vikuu.
Amewataka walimu wakuu kutotuma watoto nyumbani wakati huu kwani serikali haijakatiza mpango huo na itaendelea kufadhili watoto maskini wanaotegemea ufadhili huo wa gavana Mohamud Ali.
Mdhibiti wa bajeti Margaret Nyakango wiki jana alidai kuwa hatua ya magavana kutengea basari mgao wa kaunti ni kinyume cha sheria kwani sio jukumu la serikali za kaunti kufadhili masomo ya sekondari na vyuo vikuu.
Barile anasema kuwa endapo hilo litatendeka basi maelfu ya wanafunzi wataathirika na masomo kwani tayari wanaendelea na masomo.