Wakaazi wa maeneo ya Kambinye na Korr waishukuru ofisi ya katibu wa maeneo kame na maendeleo ya miji Kello Harsama kwa kuwapa msaada wa chakula…
February 21, 2025
Maafisa kutoka maendelo ya mradi wa Konza mamlaka ya kitaifa ya uchumi wa teknolojia kwa shirikiano na wizara ya mawasiliano na wizara ya maswala ya ndani leo imezindua ujenzi wa kituo cha mafunzo ya kiteknolojia katika eneo la shauri yako katika wadi ya Marsabit central.
Hafla hiyo imehudhuriwa na naibu kamishna wa kaunti ya Marsabit David Saruni.
Kwa mujibu wa mhandisi anayesimamia shughuli ya ujenzi amesema kuwa mradi huo utawafaidi vijana kwa masomo ya teknolojia na pia nafasi za ajira nchini.
Mradi sawia na huo umezinduliwa katika eneo la Karare. Mpango huu ni wa Serikali kuu ambapo imepanga kufanikisha mpango wa vijana kujiajiri kote nchini.