Local Bulletins

Serekali yatakiwa kutoa hamasa kwa jamii kuhusiana na ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake na wasichana nchini.

Na JB Nateleng

Serekali imetakiwa kulinda katiba pamoja na haki za wananchi wa Kenya ili kutatua mzozo ambao utasababisha maafa nchini.

Haya ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la MWADO, Nuria Gollo.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee Nuria amesema kuwa ipo haja ya serekali kuweza kutoa hamasa kwa jamii kuhusiana na haki za binadamu hii ni baada ya ongezeko la visa vya mauwaji ya wanawake na wasichana nchini.

Nuria pia amelaani kisa cha hivi punde ambapo mama mmoja aliuawa katika eneo la Badasa kaunti ya Marsabit akisema kuwa mshukiwa anafaa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Nuria ameitaka pia serekali kuweza kusikia kilio cha wananchi badala ya kuwakandamiza kwa kuwateka nyara na kuwasababishia majeraha ambayo huenda ikawasababishia pia maafa.

Mwanaharakati huyu ameichangamoto familia kuipa mazungumzo kipaumbele ili kutatua migogoro inayotokana na hali ngumu ya maisha.

Subscribe to eNewsletter