Local Bulletins

Serekali yatakiwa kuhakikisha kuwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV, ARVs,zinapatikana…

Huku serekali ya Kenya kupitia idara ya afya ikiripoti kupungua kwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV, ARVs, wanaharakati wa kutetea haki za watu wanoishi na ugonjwa wa ukimwi wameiomba serekali kuweza kubuni mbinu mbadala ya kuhakikisha kuwa upungufu huu hautaadhiri upatikanaji wa ARVs.

Wa hivi punde ni mwanaharakati Qabale Tacha ambaye ni mtetezi wa haki za watu wanoishi na ugonjwa wa ukimwi katika kaunti ya Marsabit ambaye ameitaka serekali kuhakikisha kuwa ARVs zimepatikana na kutolewa kwa zahanati pamoja na hospitali zote za serekali.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee Qabale ameiweka wazi kwamba ni jukumu la serekali kuhakikisha kuwa dawa hizi zinapatikana kwa wingi nchini ili kuwasaidia wale wanaziotegemea.

Aidha Qabale ametoa rai kwa serekali kuu na serekali ya kaunti kuweza kuwaletea chakula watu wanaoishi na virusi vya ukimwi jimboni badala ya kuwatelekeza na kuwaacha wakijing`ang`ania kukimu mahitaji yao.

Mwanaharakati huyu ameyachangamoto mashirika yasiyo ya kiserekali kuweza kujitokeza na kuwasaidia watu kwa kutoa hamasa kuhusu kujua hali yao ya HIV na pia kuwahimisa wanaoishi na virusi hivi kuendelea kutumia dawa za ARVs.

Wiki hii, mwenyekiti wa shirika la linalowaleta pamoja watu wanaosihi na virusi vya ukimwi nchini National Empowerment Network of People Living with HIV/AIDS in Kenya (Nephak) Nelson Otwoma alisema kuwa kwa sasa usambazaji wa ARV unatosha hadi mwezi Julai mwaka huu huku hatma ya upatikanaji wake baada ya muda huo ukiwa haujulikani.

Subscribe to eNewsletter