Wakaazi wa Marsabit wakerwa na hatua ya kuahirishwa kwa vikao vya kutoa maoni bila kujulishwa mapema.
February 20, 2025
Na Isaac Waihenya,
Serekali ya kaunti ya Marsabit imetakiwa kuangazia kikamilifu maswala yanayowaadhiri vijana hapa jimboni.
Haya yamekariri na kiongozi wa vijana katika eneo bunge la Saku Abdiaziz Boru.
Akizungumza na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee, Boru amepuzilia mbali ripoti kutoka kwa mratibu wa bajeti nchini, Magreat Nyakang’o iliyoonyesha kuwa kaunti ya Marsabit inaongoza kati ya kaunti ambazo zilitenga angalau asilimia 30 ya fedha na kuzielekeza kwa maendeleo, Boru ametaja kwamba vijana hapa jimboni wameachwa nje katika mipango ya serekali.
Aidha Boru ameitaka serekali kuhakikisha kwamba vijana wanahusishwa kikamilifu katika mgao wa bajeti,jambo ambalo litapunguza baadhi ya changamoto zinazowakumba vijana ikiwemo utumizi wa dawa za kulevya.
Kadhalika Boru ameitaka serekali kuhakikisha kwamba inakamilisha uwanja wa michezo wa Marsabit ili kuwapa vijana nafasi ya kukuza talanta zao.