Serekali yatakiwa kutoa hamasa kwa jamii kuhusiana na ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake na wasichana nchini.
January 28, 2025
Na Samuel Kosgei
Rais William Ruto leo amekuwa mwenyeji wa viongozi wa Umoja wa Afrika katika mkutano jijini Nairobi ili kuratibu mikakati ya maendeleo iliyoainishwa chini ya Mageuzi ya Kimuundo ya Umoja wa Afrika.
Ruto amesisitiza hitaji kubwa la mabadiliko barani, akibainisha kuwa Afrika inakabiliana na changamoto za kiuchumi, maendeleo ya kijiografia, na mabadiliko ya kijamii yasiyokuwa na kifani.
Akitaja kuwa migogoro inagharimu bara hili shilingi trilioni 2.325 kila mwaka, Kiongozi wa Taifa aliongeza kuwa mfumo wa usalama unapaswa kuimarishwa ili kufanikisha amani katika mataifa yanayokumbwa na vita.
Rais Ruto amesikitikia hali ya usalama katika taifa la Congo haswa ukanda wa mashariki ya DRC ambako waasi wa M23 wametawala na kusababisha machafuko makali kati ya jeshi la serikali na waasi.
Amesema tayari ameitisha kikao cha dharura na marais wa ukanda wa afrika mashariki siku ya Jumatano ili kujadili mzozo wa taifa la DR Congo.