Local Bulletins

Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.

NA COROL WAFORO

Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.

Akithibitisha kisa hicho Chifu wa Laisamis Agostine Supeer amesema kuwa mwanaume huyo alijifungia nyumbani kwake na kujinyonga kutumia nyaya za stima.

Mkewe mwanaume huyo alipiga kamsa ambapo wakaazi walifika nyumbani kwao na kumwokoa mumewe.

Inakisiwa kuwa jaribio hilo la kujitoa uhai ni kutokana na mzozo wa kinyumbani pamoja na msongo wa mawazo.

Chifu Supeer ametoa rai kwa wananchi kutafuta ushauri wanapokabiliana na matatizo yoyote.

Mwanaume huyo amelazwa katika hospitali ya Laisamis ambapo anaendelea kupokea matibabu.

Subscribe to eNewsletter