Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Na Henry Khoyan
Mwanafunzi mmoja wa Shule ya Msingi ya Karare ameaga dunia ghafla leo Alhamisi alipokuwa akielekea shuleni na wenzake.
Chifu wa eneo hilo, Magdalene Ilimo, amedhibitisha kuwa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14 alizirai ghafla walipokuwa barabarani kuelekea shuleni na wenzake.
Wenzake walikimbia nyumbani kutoa ripoti ya tukio hilo. Chifu amesema mwanafunzi huyo alifariki alipofikishwa Hospitali ya Rufaa ya Marsabit.