Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Na Samuel Kosgei
MWAKILISHI wa wanawake kaunti ya Marsabit Naomi Jillo Waqo ameelezea haja ya kuimarisha hazina ya pesa za kusawazisha maendeleo (equalization fund) katika kaunti za maeneo kame na zilizobaki nyuma.
Naomi akiunga mkono mjadala wa mswada huo bungeni amesema kuwa kuna haja ya kaunti zilizosalia nyuma kupewa pesa hizo ya kusawazisha maendeleo kwani kwa muda kaunti za maeneo kame kama vile Marsabit imesalia nyuma kwa muda mrefu.
Amesema kuwa magavana wa kaunti hizo wanafaa kutumia pesa hizo kupeleka maendeleo mashinani haswa itatue shida kama vile maji, hospitali na hata barabara za mashinani.
Hata hivyo Naomi ameonya magavana dhidi ya kutumia vibaya pesa hizo za nyongeza kwani kwa muda pesa hizo kazi yake haionekani. Anasema katika kaunti nyingine matumizi ya hela hizo huonekana japo kwingine kazi yake haionekani na wananchi.
Ametaka pia makundi yaliyosahaulika kama vile walemavu, wanawake na vijana kupewa kandarasi kwenye miradi itakayoanzishwa chini ya hazina hiyo ya equalization fund.