Local Bulletins

Msitu wa Marsabit umeweza kuongezeka kulingana na idara ya misitu (KFS) Marsabit

NA JB NATELENG

Msitu wa Marsabit umeweza kuongezeka kwa mwaka mmoja uliopita na hili limeafikiwa baada ya ushirikiano wa idara ya misitu (KFS) pamoja na  washikadau na wakazi wa Marsabit

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, msimamizi wa msitu Marsabit Kadiro Oche amesifia ushirikiano ambao umekuwepo kati ya KFS na wananchi wa Marsabit akiwataka kuzidisha bidii ya kupanda miti na kutunza kwa manufaa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kadiro amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuweza kuhakikisha kuwa ameshiriki kikamilifu katika kuboresha misitu.

Kadiro amesema kuwa idara hiyo itashirikiana na jamii zinazoishi karibu na msitu msimuu huu wa kiangazi ili kutoa ratiba ya jinsi na ambavyo watakuwa wakiwanyeshwa mifugo ama kuteka maji kwenye msitu.

Aidha Kadiro amewarai wakazi wanaoishi karibu na mizitu kuasi tabia ya kuwasha moto karibu na misitu ili kuepuka kusababisha hasara ya msitu kuchomeka.

Subscribe to eNewsletter