Wakaazi wa Marsabit wakerwa na hatua ya kuahirishwa kwa vikao vya kutoa maoni bila kujulishwa mapema.
February 20, 2025
NA CAROLINE WAFORO
Kwa muda mrefu kaunti za wafugaji katika eneo pana la Kaskazini Mashariki zimekumbwa na changamoto ya uhalifu wa wizi wa mifugo ambao umehusishwa haswa na Warani kutoka jamii mbalimbali.
Hata hivyo hali hii imeonekana kubadilikwa kwa pakubwa baada ya baadhi ya vijana hao kujiunga na chama cha kutoa akiba na mikopo cha Rangelands Sacco chini ya shirika lisilo la kiserikali la NRT ambacho kimewasaidia katika kujihusisha na biashara halali.
Haya ni kulingana na Peter Nguno ambaye ni afisa mkuu wa kitengo cha biashara katika Rangelands Sacco ambaye amezungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kila mwaka wa wajumbe wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Archers Post kaunti ya Samburu.
Nguno anasema kuwa miradi wanayoifanikisha inawasaidia vijana kuasi uhalifu.
Aidha amewataka vijana kujiunga na chama hicho akisema kuwa itakuwa suluhu kwa uhalifu huo katika kaunti za wafugaji ikiwemo kaunti ya Marsabit.
Matamshi yake yamekaririwa na afisa mwenzake Stephen Seboku.
Vile vile amesema kuwa wanawasaidia kina mama katika kuendesha biashara mbalimbali zinazowasaidia katika kujikimu kimaisha.
Rangelands sacco inajumuisha wanachama 6,400 kutoka kaunti zilizooko maeneo kame na zile za pwani.
Wakati uo huo Chama cha akiba na mikopo cha Rangelands chini ya mwavuli wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Northern Rangelands Trust (NRT) kimezidi kutoa mafunzo kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusiana na mikakati ya kutunza mazingira.
Mwenyekiti wa hifadhi ya Jaldesa kutoka jimbo la Marsabit Galgallo Arero ameeleza jinsi miradi mbalimbali chini ya shirika hili inasadia jamii pana ya Marsabit katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Kwa muda mrefu eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya limekuwa likikabiliana na uhalifu wa wizi wa mifugo ila chama hiki cha akiba sasa kinabadilisha maisha ya vijana katika kaunti mbalimbali sasa wakiasi uhalifu na kukumbatia biashara.
Paramase Lesanangi kutoka Oldonyiro kaunti ya Isiolo ni mwananchama wa Rangelands Sacco na ambaye alikuwa morani ila sasa ni mwanabiashara.
Paramase anasema kuwa maisha yake yamechukua mkondo tofauti akitoa rai kwa vijana wenzake kuasi uhalifu wa wizi wa mifugo.
Kina mama pia hawajasazwa nyuma wakisema kuwa mikopo wanayopokea kutoka chama hicho imewasaidia katika kujitegemea kimaisha. Nabiki Lesuper kutoka hifadhi ya Karama kaunti ya Samburu anasema kuwa hilo limepunguza migogoro ya kinyumbani.
Naye Rukia Gafo kutoka kaunti ya Tana River ametoa wito kwa vijana kuweka akiba.